About Me

i am swalwhe kiluvia ,i would like to have defefernt frends to share idea

Friday, November 19, 2010

Hongera wawezeshaji

Nilipoanza mafunzo mafupi ya waandishi wa habari mnamo tarehe 15 nov hadi hii leo tarehe 19 nov  2010 sikuwa na ufahamu wa kutosha katika kutembelea mitandao mbalimbali yaani Web Site ili kutafuta habari na kuweza kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na waandishi wenzangu wa habari.

Hata hivyo kwa hivi sasa baada ya kozi hii ya kutumia mtandao ,yaani internet,chini ya wezeshaji wetu hususan Peik Johansson  kutoka katika taasisi ya VIKES The finnish foundation for media,communication and development alituelekeza namna ya kufungua blogs zetu na kutembelea katika tovuti mbalimbali.

Lakini sio Johansson peke yake ,pia tmekuwa muwezesha ambaye ni muandikaji maarufu hapa nchini wa makala Majid Mjengwa ambaye pia ametufundisha mengi ,ikiwemo kundaa vema tovuti zetu blogs.

Hakika tumeyafurahia sana mafunzo haya ,na ninaimani kuwa washiriki wote wa mafunzo haya ,hakuna alietoka kapa,.shukurani za pekee kwa Missa tan na Vikes  la nchini Finland kwa kutuandalia mafunzo haya adhim.

No comments:

Post a Comment