About Me

i am swalwhe kiluvia ,i would like to have defefernt frends to share idea

Thursday, November 18, 2010

Ahamed Khalifani Ghailani

Mahakama ya kiraia nchini marekani ,imeuingiza hatiani  raia wa Tanzania Ahamed Khalifani ghailani kwa kula njama ya kushambulia kwa bomu mali ya taifa la marekani
Ghailani alishitakiwa kwa kosa la kuhusika katika mashambulizi ya kundi la kigaidi la alkaida  dhidi ya ubalozi wa marekani nchini kenya na Tanzania mwaka 1998 ambapo katika tukio hilo walifariki watu 224
Katika taarifa hiyo inasema ghailani alichangia kwa kiasi kikubwa maandalizi na mipango ya kulipuo ubalozi huo nchini Tanzania na kenya,kwa kununua mitungi na ya gesi zilizolipuka pamoja na lori lilobeba milipuko hiyo.
Hata hivyo ushahidi uliowasilishwa na upade wa ushahidi mbele ya mahakama hiyo ya marekani ,zimekataliwa kwa kuwa zimekusanywa na maafisa wa ujasusi wa marekani kwa njia isiofaa,hivyo kumpata na hatia ya kosa moja ya kupanga kuharibu mali ya majengo ya serikali
Maafisa hao wa ujasussi wanadaiwa kutumia mbinu ya kumuhoji mshukiwa kwa kutumia njia ya kumtesa kutoa habari  na kukiri mashtaka.

No comments:

Post a Comment