About Me

i am swalwhe kiluvia ,i would like to have defefernt frends to share idea

Sunday, November 6, 2011

NI lINI WANAHABARI MTAJIKOMBOA ?


Kuwepo kwa vyombo vingi vya habari hapa nchini Tanzania kuanzia miaka ya 80 kulipokelewa kwa mikono miwili na kuwepo kwa matumaini makubwa ya kupata malipo yaliyo bora lakini kinyume chake tumeshuhudia vyombo hivyo haviwanufaishi walengwa badala yake vinazidi kuwanyonya na kuwakandamiza na kudumaza taaluma na ufanisi .
Siku zote kumekuwepo na juhudi zinazofanywa na wanaharakati wanaotetea uhuru wa habari lakini hawajahi kutokea kutetea masilahi  na haki sitahili za mwanahabari ambae kukiwa na shida anaonekana ni muhimu  lakini tatizo linapokwisha hakumbukwi .
Cha kushangaza ni kuwa wanaharakati hao ambao tumekuwa tukiwashuhudia kushika mabango juu ya mambo  mbalimbali ya ukandamizaji yanapotokea katika taasisi au jamii fulani,wameshindwa kugeuza mabango hayo kuwateta wanahabari dhidi ya wamiliki wa vyombo hivyo ambao wanajiona ni sawa na miungu watu hawako tayari kutoa maslahi yaliyo bora kwa wanahabari.
kukosekana kwa chombo cha kutetea masilahi ya wanahabai kumesababisha kuwepo kwa rushwa  miongoni mwa wanahabari hasa wahariri ili kuweza kujikimu kimaisha hali ambayo ni hatari kwa utoaji wa habari za haki na ukweli ambazo haziegemei upande wowote wa jamii.
Ukiuliza wanahabari wanamtumikia nani jawabu lake ni moja tu ambalo ni rahisi sana watasema wanamtumikia  mwanasisa na mfanyabiashara kwa ajili ya masilahi ili kupata payola, na sio jamii kama wengi wanavyofikiri.

DEMOKRASIA SIO VURUGU.

KUWEPO kwa vyama vingi vya siasa katika mataifa mbalimbali barani Afrika hasa yanayoendelea ni utamaduni mpaya ambao waafrika wameshindwa kuutumia kama ipasavyo na badala yake  mfumo huo unatumika kama sehemu ya vurugu na kulipiziana visasa na kukomoana.
 Tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara kuwepo kwa mwingiliano au uvamizi wa chama kimoja kuvamia eneo ,mashina ya wakereketwa, wafurukutwa au maskani ,ambayo ni  ngome ya chama kingine kwa kisingizio cha kutafuta wafuasi na  kufungua matawi hapo jirani hii inaonysha wazi kuwa wahusika hawajakomaa kisiasa.
Mfano wa hivi karibuni ni chama kimoja chaupinzani kaskazini mwa Tanzania, kilivamia katika eneo la chama tawala na kung;oa mlingoti wa bendera ya chama tawala na kupora bendera kasha kubadilisha shina na kupandisha bendera ya chama hicho hali iliyopelekea wafuasi wanane wa chama hicho cha upinzani kukamatwa na polisi.
Jehiyo ndio demokrasia ya vyam vingi? Au huo ni uchanga wa kisiasa?je siasa za aina hii zinatrupeleka wapi,akili ya kuambiwa changanya na yako wahenga walisema.

Sunday, October 30, 2011

DEMOKRASIA NI JANGA AFRIKA

Demokrasia katika nchi za kiafriika inakuwa ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha sana, kwa kuwa inatumika kuleta machafuko na ghasia ambazo hupelekea  mamia na maelfu ya watu kupoteza maisha yao na pia kuharibu uchumi wanchi na watu , hususan kina mama na watoto hiutaabika sana.
Wengi wa wanasiasa  huwa na ubinafsi haramu, kwa kuwa hutumia damu za watu ili kujitafutia umaarufu na ushujaa ilihali wahanga wa wanasiasa hao husahalika maratu wanapozikwa, utwashangaa wanasiasa hao  baada ya mauaji ya raia wao hukaa meza moja na mahasimu wao wakipata shushu huku raia wakipotea muelekeo kwakuwa kutokana na fitna za wanasiasa huwasababishia kupoteza uchumi wao hata ule mgodo walio kuwa nao kwa nini hawakaa kabla ya kuleta madhara?
Ni vema wananchi kuwa macho na wanasiasa hawa uchwara ambao hutumia kigezo cha demokrasia kwa kupalilia vyeo vyao na vitambi vyao bila kujali maisha ya watu mali zao kwa kupandiza ugomvi na fitna ili  kugombanisha watu kwa manufaa yao binafsi.
Wanasiasa wengi wa waafrika huenda kinyume na falsafa wa Raisi wa zamani wa marekani aitwaye John Kennedy, kwa kifupi alifahamika kwa J.F.K alisema kabla ya kugombea uongozi ni vema kujiuliza utifanyia nini nchi yako badala ya kusema nchi yako itakufanyia nii, lakini lakushangaza na kustaajabisha ni kwamba vionozi wengi wa kiaafrika hutafuta madaraka kwa nguvu kwa minajili ya kujilimbikizia mali na kutafuta ukubwa bila kujali maisha au mali za watu kiasi gani zaweza kuteketea kwa kupitia choko choko zao , huku wao wenyewe hukimbilia nchi nyengine mambo yakiharibika.
Napenda kutoa mfano halisi ni tukio ambalo lilitokea ya hivi karibuni kaskazini mwa Tanzania  ambapo kiongozi mmoja wa kisiasa aliwashawishi wafuasi wake kwenda katika kituo cha polisi kutoa baadhi ya viongozi waliokuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kwa ukkufanya maandamano bila kuwa na kibali, kauli ya mwanasiasa huyo ilikua kama ifuatavyo napenda kunukuu baadhi ya maneno ‘haya wote tuondoke hapa kwa pamoja twende tukawatoe viongozi wetu katika kituo cha polisi, kina mama na watoto waende nyumbani haya twendeni moja, mbili, tatu twende!!!’ lakini chakushangaza hapakuwepo na kiongoz hata i mmoja alieandamana na wafuasi hao. Kila mmoja alitafuta njia yake wengine walikimbilia mahotelini na wengine majumbani. Huku watu wengine wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa Je hi I ndo sawa?
Napenda kutumia fursa hii kuwashauri wananchi wezangu, akili za kuambiwa changanya na zako.