VETI FEKI SIO JISHINI PEKE YAKE
Suala la veti bandia ni janga la taifa, wafanyakazi wengi katika tasisi nyingi serikalini wanatumia vyeti hivyo,hii nichangamoto kubwa kwa serikali kufuatilia kwa kina suala hili.
mali ya nchi ni watu
mwanga wa jamii
About Me
- kiluvia
- i am swalwhe kiluvia ,i would like to have defefernt frends to share idea
Wednesday, May 16, 2012
Sunday, November 6, 2011
NI lINI WANAHABARI MTAJIKOMBOA ?
Kuwepo kwa vyombo vingi vya habari hapa nchini Tanzania kuanzia miaka ya 80 kulipokelewa kwa mikono miwili na kuwepo kwa matumaini makubwa ya kupata malipo yaliyo bora lakini kinyume chake tumeshuhudia vyombo hivyo haviwanufaishi walengwa badala yake vinazidi kuwanyonya na kuwakandamiza na kudumaza taaluma na ufanisi .
Siku zote kumekuwepo na juhudi zinazofanywa na wanaharakati wanaotetea uhuru wa habari lakini hawajahi kutokea kutetea masilahi na haki sitahili za mwanahabari ambae kukiwa na shida anaonekana ni muhimu lakini tatizo linapokwisha hakumbukwi .
Cha kushangaza ni kuwa wanaharakati hao ambao tumekuwa tukiwashuhudia kushika mabango juu ya mambo mbalimbali ya ukandamizaji yanapotokea katika taasisi au jamii fulani,wameshindwa kugeuza mabango hayo kuwateta wanahabari dhidi ya wamiliki wa vyombo hivyo ambao wanajiona ni sawa na miungu watu hawako tayari kutoa maslahi yaliyo bora kwa wanahabari.
kukosekana kwa chombo cha kutetea masilahi ya wanahabai kumesababisha kuwepo kwa rushwa miongoni mwa wanahabari hasa wahariri ili kuweza kujikimu kimaisha hali ambayo ni hatari kwa utoaji wa habari za haki na ukweli ambazo haziegemei upande wowote wa jamii.
Ukiuliza wanahabari wanamtumikia nani jawabu lake ni moja tu ambalo ni rahisi sana watasema wanamtumikia mwanasisa na mfanyabiashara kwa ajili ya masilahi ili kupata payola, na sio jamii kama wengi wanavyofikiri.
DEMOKRASIA SIO VURUGU.
KUWEPO kwa vyama vingi vya siasa katika mataifa mbalimbali barani Afrika hasa yanayoendelea ni utamaduni mpaya ambao waafrika wameshindwa kuutumia kama ipasavyo na badala yake mfumo huo unatumika kama sehemu ya vurugu na kulipiziana visasa na kukomoana.
Tumekuwa tukishuhudia mara kwa mara kuwepo kwa mwingiliano au uvamizi wa chama kimoja kuvamia eneo ,mashina ya wakereketwa, wafurukutwa au maskani ,ambayo ni ngome ya chama kingine kwa kisingizio cha kutafuta wafuasi na kufungua matawi hapo jirani hii inaonysha wazi kuwa wahusika hawajakomaa kisiasa.
Mfano wa hivi karibuni ni chama kimoja chaupinzani kaskazini mwa Tanzania, kilivamia katika eneo la chama tawala na kung;oa mlingoti wa bendera ya chama tawala na kupora bendera kasha kubadilisha shina na kupandisha bendera ya chama hicho hali iliyopelekea wafuasi wanane wa chama hicho cha upinzani kukamatwa na polisi.
Jehiyo ndio demokrasia ya vyam vingi? Au huo ni uchanga wa kisiasa?je siasa za aina hii zinatrupeleka wapi,akili ya kuambiwa changanya na yako wahenga walisema.
Sunday, October 30, 2011
DEMOKRASIA NI JANGA AFRIKA
Demokrasia katika nchi za kiafriika inakuwa ni jambo la kusikitisha na kuhuzunisha sana, kwa kuwa inatumika kuleta machafuko na ghasia ambazo hupelekea mamia na maelfu ya watu kupoteza maisha yao na pia kuharibu uchumi wanchi na watu , hususan kina mama na watoto hiutaabika sana.
Wengi wa wanasiasa huwa na ubinafsi haramu, kwa kuwa hutumia damu za watu ili kujitafutia umaarufu na ushujaa ilihali wahanga wa wanasiasa hao husahalika maratu wanapozikwa, utwashangaa wanasiasa hao baada ya mauaji ya raia wao hukaa meza moja na mahasimu wao wakipata shushu huku raia wakipotea muelekeo kwakuwa kutokana na fitna za wanasiasa huwasababishia kupoteza uchumi wao hata ule mgodo walio kuwa nao kwa nini hawakaa kabla ya kuleta madhara?
Ni vema wananchi kuwa macho na wanasiasa hawa uchwara ambao hutumia kigezo cha demokrasia kwa kupalilia vyeo vyao na vitambi vyao bila kujali maisha ya watu mali zao kwa kupandiza ugomvi na fitna ili kugombanisha watu kwa manufaa yao binafsi.
Wanasiasa wengi wa waafrika huenda kinyume na falsafa wa Raisi wa zamani wa marekani aitwaye John Kennedy, kwa kifupi alifahamika kwa J.F.K alisema kabla ya kugombea uongozi ni vema kujiuliza utifanyia nini nchi yako badala ya kusema nchi yako itakufanyia nii, lakini lakushangaza na kustaajabisha ni kwamba vionozi wengi wa kiaafrika hutafuta madaraka kwa nguvu kwa minajili ya kujilimbikizia mali na kutafuta ukubwa bila kujali maisha au mali za watu kiasi gani zaweza kuteketea kwa kupitia choko choko zao , huku wao wenyewe hukimbilia nchi nyengine mambo yakiharibika.
Napenda kutoa mfano halisi ni tukio ambalo lilitokea ya hivi karibuni kaskazini mwa Tanzania ambapo kiongozi mmoja wa kisiasa aliwashawishi wafuasi wake kwenda katika kituo cha polisi kutoa baadhi ya viongozi waliokuwa wakishikiliwa na jeshi hilo kwa ukkufanya maandamano bila kuwa na kibali, kauli ya mwanasiasa huyo ilikua kama ifuatavyo napenda kunukuu baadhi ya maneno ‘haya wote tuondoke hapa kwa pamoja twende tukawatoe viongozi wetu katika kituo cha polisi, kina mama na watoto waende nyumbani haya twendeni moja, mbili, tatu twende!!!’ lakini chakushangaza hapakuwepo na kiongoz hata i mmoja alieandamana na wafuasi hao. Kila mmoja alitafuta njia yake wengine walikimbilia mahotelini na wengine majumbani. Huku watu wengine wakipoteza maisha na wengine kujeruhiwa Je hi I ndo sawa?
Napenda kutumia fursa hii kuwashauri wananchi wezangu, akili za kuambiwa changanya na zako.
Saturday, December 11, 2010
CHADEMA MTIHANI ZITO
KUMBE UONGOZI CHADEMA NI MTIHANI MZITO ZITO
Mgogoro wauongozi ndani yachadema ulianza punde tu baada ya Zito Zuberi Kabwe kutangaza zamira yake yake ya kugombea nafasi ya uwenyekiti wa chama hicho jambao ambalo liliibua sintofahamu kati yake na mwenyekiti alioko madarakani Freeman Mbowe.
Sakata hili lililazimu baadhi ya wazee akiwemo inayesemekana kuwa mkwe wa Feeman Mbowe ambaye pia ni muasisiswa chama hicho Ediwini kutoa msimamo mkali kuamuru Zito kabwe atoa jina lake mara moja ,lakini hata hivyo Zito alikuwa ngangari nakutoamsimamowake kuwa asingetoa kwa kuwa anatumia haki yake ya kidemokrasia.
Lakini mambo yalizidi sana na kuona kumbe ndani ya chama chake hakuna demokrasiaaliamua kuachia ngazi ,ndipo walipomuahidi kumpa cheo cha ukatibu mkuu,lakini hata hivyo walimpa cheo cha naibu katibu mkuu.
Lakini mambo hayakuishia hapo baada ya uchaguzi wa Urais na Ubunge wa mwka huu 2010 kumalizika pia Zito alitangaza dhamira yake yakutaka kugombea kuwa kiongozi wa upinzani bungeni,lakini ilionesha dhahiri mwenyekiti wake Mbowe hakuridhika kumuunga mkono na nakumbidi kutoa kauli yakuwa mchakato wakupata kiongozi huyo utajadiliwa na chama.
Lakini tulichokiona baadae ni kuonaMbowe ndie alichaguliwa kuwa kiongozi wa upinzanibungeni na Zito Kabwe kuwa naibu wake,wachambuziwamambo husema kupata cheo hichopengine alitumia fedha zake katikakuwafadhili baadhi yawabunge wakati wa kampena hivyo walifanya hivyo kulipa fadhila.
Kitendo cha Zito kuomba kiti hicho pia wachambuzi hao wameelezea pengine imeongeza hasira za Mbowe hivyo kuenda mbali zaidi kutumia wabunge walealiowadhamini kuhakikisha wanamnyangaya hata nafasi ya unaibu katiaka kamba ya upinzani bungeni kupitia chadema nap engine kumfukuza uanachama.
Chama hakijaweka utaratibu wa namna kiongozi wa upinzani bungeni anapatikana. Utaratibu ukishawekwa nitatoa taarifa rasmi ila kwa sasa pitia Facebook yangu utaona ujumbe wangu,” alisema Zito
Mwenyekiti huyu wa chadema hakuanza mgogoro wa watu waonataka kugombea uongozi na Zito Peke yake, lakini pia alikugombana na alikuwa makamu mwenyekuti wa chama hicho Chacha Wange,Devid Kafulila na viongozi wengine ambao walijiondoa chadema na kudaikuwa chama hicho kinaongozwa na watu wawili kama kamuni yao.
Chacha wange yeye kizazaa kilibuka alipo hojii matumizi ya Ruzuku napia kutangaza nia yake ya kuta kugombea nafasi ya uwenyekiti katika chama hicho,hali ambayo ilisababisha mtafarukuhadi kifo chake ambacho kilizua utata alipo kuwa akirejea bungeani dodoma july 2008.
Friday, November 19, 2010
Hongera wawezeshaji
Nilipoanza mafunzo mafupi ya waandishi wa habari mnamo tarehe 15 nov hadi hii leo tarehe 19 nov 2010 sikuwa na ufahamu wa kutosha katika kutembelea mitandao mbalimbali yaani Web Site ili kutafuta habari na kuweza kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na waandishi wenzangu wa habari.
Hata hivyo kwa hivi sasa baada ya kozi hii ya kutumia mtandao ,yaani internet,chini ya wezeshaji wetu hususan Peik Johansson kutoka katika taasisi ya VIKES The finnish foundation for media,communication and development alituelekeza namna ya kufungua blogs zetu na kutembelea katika tovuti mbalimbali.
Lakini sio Johansson peke yake ,pia tmekuwa muwezesha ambaye ni muandikaji maarufu hapa nchini wa makala Majid Mjengwa ambaye pia ametufundisha mengi ,ikiwemo kundaa vema tovuti zetu blogs.
Hakika tumeyafurahia sana mafunzo haya ,na ninaimani kuwa washiriki wote wa mafunzo haya ,hakuna alietoka kapa,.shukurani za pekee kwa Missa tan na Vikes la nchini Finland kwa kutuandalia mafunzo haya adhim.
Thursday, November 18, 2010
world trade center
Mnamo tarehe 11 mwezi wa 9 mwaka 2001,shambulio kubwa la hatari katika nyakati za asubuhi kundi la alkaida walitumia ndege ya abiria ilikuwa imebeba wafanyabiashara na na kulilipua jingo pacha la kituo cha kibishara cha kimataifa linajulikana kama WTC lilopo katika jiji la New York .
Tukio hilo lilisababisha watu wote waliokuwepo ndani ya ndege hiyo kupoteza maisha yao nawatu wote waliekuwemo ndani ya ndege hiyo,pamoja na majengo ambayo yamelizunguka jingo hilo wikipedia http://en.wikipedia.org
kwa mujibu wa wa wizara ya afya ya marekani zaidi watu 800 walipoteza maisha yao wakiwemo wahudumu wa zima moto na askari polisi walikuwa wakitoa msaada kwa wanachi
Licha ya shambulio hilo kutokea jingo la WTC-7 halikushambuliwa na ndege yeyote lakini lilionekana kushika moto sehemu chache katika jengo hilo hususan kaskazini mwa jenjo hilo kabla ya kuangakaka. http://911research.wtc7
Subscribe to:
Posts (Atom)